Shirika la ITRASAGRI linatumia mbolea za FOMI kwa kuzalisha mbegu bora
Hapa tuko inchini Burundi Roho ya Afrika mkoani Kayanza ndipo shirika la mbegu na kilmo ITRASAGRI ,shirika lenye malengo ya kuendeleza segita ya mbegu bora na kilimo hapa burundi na sehemu zingine ambapo kampuni ya mbolea za kaboni na za kikemikali zinapatikana tayari,mbolea inayosaidia ardhi kurudisha rutuba yake na muongezeko wa mazao kwa miaka mitano tayari ili tuweze kutokomeza maradhi ya utapiamlo,njaa na umasikini hivyo tutaweza kufikia maendeleo ya kudumu tukielekea kwa kaulimbiu ya inchi ;inchi ilioendelea mnamwo mwaka wa 2040 na inchi tajiri mwaka wa 2060 tukiézingatia kuwa kilimo ni msingi wa maisha na maendeleo .Ili kilimo kiweze kutufikisha kwa malengo hayo kinatakiwa kuwa cha kisasa na ardhi iwe imeandaliwa vizuri kwa kutumia kwa usahihi mbolea bora na mbegu bora na baraka za mwenyezi Mungu zikiwemwo.
Hapa munapoona
ni taraf aya Muruta sehemu ambako kunafanyika utafiti kwa ongezeko la mbegu bora hususani kwenye mbegu ya viazi .Mukurugenzi wa shirika la kuzalisa mbegu bora na kilimo ITRASAGRI Dr Deo Guide Rurema akiongozana nawafanyakazi wenzake ,wafanyakazi wa kampuni inayotengeneza mbolea za kaboni na za kikemikali FOMI na wandishi wa habari alitembelea maeneo ili ashuhudie maendeleo ya kazi kwa miezi mitano toka shirika hilo limeanzishwa. Hapa anaanza akieleza kwa nini shirika hilo lilianzishwa na nini kazi zake
kuezesha ongezeko la mbegu bora sio kazi rahisi inahitaji ufuatiliaji wa kalibu kwa hatua mbalimbali na ukuaji wa mbegu hizo kama kwenye viazi unaanzia kwenye nyumba zilizowekwa kwa ajili ya utafiti na hatimaye kuzipanda kwenye shamba mpaka pale ambapo wanazigawa kwa wakulima . Mbegu zikitokezea kwenye nyumba za kuzizalisha ,zitapandwa kwenye mashamba munayoyaona . Shilika la kuzalisha mbegu bora na kilimo ITRASAGRI liko linafanya utafiti kwa kuzalisha mbegu bora pia kwenye tarafa ya Gahombo
sehemu yenye mashamba makubwa ya mahindi na viazi,unapoyaangalia mashamba haya ni yakuvutia na yako kwenye milima sehemu ambapo utafikiri kilimo hakiwezekani kulingana na muonekano wake
Mukurugenzi Dr Deo Guide Rurema hapa atatueleza utalaam walioutumia ili mashamba yawe mazuri na yakuvutia kama munavyoyaona : Mbolea ya FOMI unapoyitumia kwenye mashamba yako hauwezi kujutia iwe ni kwa mavuno au kwenye afya ya watu ;kwenye shirika la ITRASAGRI waliijaribu na hapa Mukurugenzi Dr Deo Guide Rurema anavionyesha kwenye mashamba ya majaribo ambapo walitumia mbolea ya FOMI
Kwenye utafiti unawofanywa na shirika la kuzalisha mbegu bora na kilimo ITRASAGRI hakusahau kuambatanisha mkulima,mufugaji na mazingira .kwenye mashamba ya utafiti utakuta wamepanda pia mti ambayo ni rafiki kwa mazao na kando ya mashamba wanamifugo pia
Kwa miezi mitano shirika la kuzalisha mbegu bora na kilimo ITRASAGRI likiwa limeanza,shirika rimesha ajiri zaidi ya wafanyakazi mia tatu ,limekuja pia kuunga mkono maendeleo ya inchi kwa kulip kodi na ushur
Hapa tuko ITRASAGRI kwa maana ya ITRACOM SEEDS AND AGRICULTURE ni center moja katika center za ITRACOM HOLDING ,hapa tuko Muruta sehemu tuko tunazalisha mbegu zisizozakawaida za awali kwenye zao la viazi,mbegu tunazozipata toka tasisi ya ISABU ili kama munavyofahamu tuweze kupata mbegu za kutosha ili tuendane na kaulimbiu ya Muheshimiwa Rais iwa inchi yetu nzuri Meja Jenerali Evariste Ndayishimiye kila mdomo upate chakula na mfuko wa kila raia upate pesa : Raia waliitikia kaulimbiu hiyo . Hapa ni vyema raia wakapate mbegu bora na wazitumie wakiwa wameweka ile mbolea nzuri ya FOMI ili mavuno yakaongezeke ;ndio maana tukichkulia mfano mzuri wa kaulimbiu ya inchi ilioendelea mnamwo mwaka 2040 na inchi tajiri mwaka 2060. Kwenye shirika la ITRASAGRI tulifurahishwa na kaulimbiu hii na kuiitikia kwa haraka na tunabahati kuwa Muheshimiwa waziri wa kilimo,mifugo na mazingira alitoa wito kwa wawekezaji ili wavunje hofu na waweze kuwekeza kwenye hii sekta ya utafiti na hapa tuliitikia wito huo ii hivi ambavyo tunavifanya viwe kiukweli msingi wa ile kaulimbiu ya kuwa inchi tajiri,inchi yenye kujitoshereza kwa chakula ,inchi yenye raia wanaofurahia kuijenga inchi yao .Huu ndio wito tuliowuitikia na tukaja kureta mchango wetu hapa kwenye majumba ya kuzalisha mbegu bora kunafanyika utafiti kama vile unavyofanyika ISABU na tulikuja kusapoti ISABU kwa hili swala la utafiti tukiitikia wito wa Me raisi kwa wawekezaji wenye uwezo kuja kuwekeza kwenye sekta ya utafiti. Muonapo viazi vikiwa kwenye stedi hii siyo kazi rahisi ni kama vile unavyolea mtoto hadi utu wake mzima . Hivi viazi munavyoona tulivileta vikiwa na sizi ndogo ilio chini ya minyoo lakini kama mulivyoshuhudia kwanza inabidi mtu we na bidii ya ufuatiliaji,awe na uwezo awe pia na utalaam ;vinahitaji usafi wa hali ya juu ili maeneo ya uzalishaji wa mbegu tuyalinde magonjwa na tunapoambatanisha hayoyote tunakua tuko kwenye hatua nzuri
Sio kwamba tunataka kuzalisha mbegu na kuzisambaza kwa raia tu tunahitaji kua na huu utalaam wa kufanya kilimo cha kisasa,kutengeneza carves ngazi maeneo yenye mitremuko ili tuishikilie rutuba hili linalohusu kuweka kwa usahihi mbolea ya FOMI,hili linalohusu kumagilia mashamba wakati wa kiangazi na tutaweza kutumia mashini za kilimo na tunahitaji kuwa mfano na kuchkuwa mstari wa mbele ili raia waweze kuja kujifunza hivyo mavuno yaendelee kuongezeka ;jambo jigine,baada ya mavuno kuongezeka pale ambapotutakua tuko tunatumikia na yakawa mengi pia kwa raia,tunatamani kuweka utalaamu wa kuwubadili na kuwufungasha kama ilivyowito wa Muheshimiwa Raisi ili tuwetunawuuzisha na sisi tupate chakula,tupte ziada ya kuuzisha inje ili tupate fedha za kigeni
Mbolea ya FOMI,ili iwe mbolea tunayoitumia hapa ni mbolea yenye manufaa mno , moja kwa mazingila,mbolea ya FOMI ina mbolea ya kemikali ambayo imechanganywa na mbolea asilia na hapo mutaelewa kuwa wanaelekeza kutotumia sana mbolea ya kikemikali ili tuwe tunatumia mbolea ambayo hayiharibu ardhi ;pili ni kwamba hii mbolea ya FOMI inakuwa na mbolea ya samadi ambayo ndani yake kwa sababu ya hiyo wadudu ambao wako ardhini wataendelea kua na uhai na mumea pia kuweza kustawi ?Mbolea ya FOMI imeeneza hayo yote ambayo nimetoka kuyataja na utumiapo mbolea ya FOMI mimea kwa kukuwa kwake huvuta ile chumvichumvi ndio maana ile chumvichumvi inasambaa kwa zao husika iwe kwa viazi,kwa mahindi,iwe ni kwa mchele au kwa ngano . Ikiwa tumetumia mbolea za kikemikali pekee,tunapokula mazao inaweza ikasababisha magonjwa kama kansa. Kwa hivyo sasa mtaelewa ya kua mbolea ya FOMI inatunza rutuba ya ardhi,inatunza afya ya watu na kutunza pia mazingira . Ukiangalia huu mmea wa mahindi,ni mmea wa kuridhisha nawakuvutia hii inadhihirisha kwamba mmea huu ulipata chumvichumvi ya kutosha ni hio chumvchumvi ni ile mbolea ya FOMI ambayo tukotunaitumia na kingine ukiona mmea umeota kwenye sehemu ambapo ardhi inageuka kua nyeusi hii inamaanisha kua mbolea ya FOMI inachanganyika na ardhi hivyo iwezeshe ardhi kubaki bora na mimea iendelee kusitawi ; jambo jingine ni rangi ya mahindi ambalo ni la kijani hii inamaanisha kwamba tumerudi zile nyakati zazamani ambapo walikua wanakuza mahindi kwa kutumia mbolea ya samadi na wakati ule mashamba yalikua na rangi hii
kama mulivyoshuhudia hapa kwenye mashamba tunapotumikiakote kunakua na miti,hapa tunataka kua mfano mzuri wa kuambatanisha kilimo,mifugo,muliona kua sehemu ya mifereji tulipanda nyasi ya kuwalisha ng’ombe hivyo kilimo,ufugaji na mazingia vifanyike kwa pamoja ili hii ardhi ambao tulirithi toka kwa mababu zetu na sisi tupate cha kuwarithi watoto na wajukuu .