Kipindi cha 1
Kiwanda cha FOMI kina makao makuu yake Maramvya,Zone ya Mutimbuzi, wilaya ya Ntahangwa, mkoa wa Bujumbura. Kiwanda hicho kilianza shughuli zake mwaka wa 2019 na kinapatikana karibu ya kiwanja cha ndege cha kimataifa Melchior NDADAYE. FOMI ni kifupi cha maneno ya kifaransa Fertilisants Organo-Mineraux na tafsiri yake ikiwa ni mcanganyiko wa mbolea asilia na mbolea ya madini. FOMI ni kiwanda kinachotengeneza mbolea za kikaboni na madini.

Mbolea hizo ni za kipekee na umahiri wake umesababisha zikapendwa na wakulima wa Burundi na wale wa nchi zingine nyingi. FOMI inatengeneza aina tatu ya mbolea : FOMI Imbura ambayo hutumika wakati wa kupanda kwa mazao kama yote. FOMI Bagara inayotumika kwa mazao yenye mzizi na mizizi wakati wa kupalilia, FOMI Totahaza inayotumika kwenye mazao ya nafaka wakati wa kupalilia.
Pamoja na aina tatu za mbolea, FOMI inatengeneza pia chokaa ya kilimo ambayo watalaamu wa maswala ya kurutubisha ardhi wanashahuri iwekwe mwezi mmoja kabla ya kupanda. Katika kipindi cha miaka 7 FOMI iliweza kutengeneza hizo aina tatu za mbolea na choka aya kilimo. Wakulima wanaridhishwa na mbolea hizo ambazo zilipelekea uzalishaji wa kilimo kuongezeka na zikarudisha rutuba ya ardhi. Kwenye maandishi yetu ya badae tutawambia haswa jinsi FOMI ilivyowezesha ardhi inayozalisha zaidi kutunzika.