Wakati huu wakulima wako wanajiandaa kwenye musimu wa kilimo A. Mukulima anaejiandalia musimu wa kilimo A, asisahau utumiaji wa chokaa ya kilimo. Munaweza mukajiuliza umuhimu wa chokaa ya kilimo ni upi? Kama inavyoelezwa na watalaamu kuhusu utumiaji wa mbolea, chokaa ya kilimo ni tofauti na aina zingine za chokaa. Kaboneka Salvator ni mwalimu chuo kikuu na ni mutalaam kwenye maswala ya kutumia mbolea anaeleza kwamba chokaa ya kilimo ni chokaa yenye chumvichumvi cha Kalisiamu(CaO)na magnesiamu(MgO). Chumvichumvi hizo ndizo pekee zinazoweza kupambana na asidi mbaya inayofahamika kama aliminiamu. Kaboneka Salvator anashahuri wakulima kuandaa vizuri mashamba, kuweka chokaa ya kilimo angalau mwezi mmoja kabla ya kupanda. Kando na kuweka mbolea ya kilimo, mtalaamu huyo anatoa wito kwa wakulima kufutilia pia ushahuri na utalaamu wanaopewa na mafundi shamba. Fahamu kwamba kiwanda cha FOMI kinatengeneza chokaa ya kilimo ambayo ni bora wakitumia utalaamu unaokubalika na kwamba kila mukulima anaeyihitaji anaweza akayipata.
