Ardhi yetu ilipoteza rutuba na ikapelekea kupoteza uwezo wake wa kuzalisha.Kupoteza rutuba kulisababishwa na kutohifadhi mazingira vizuri,kutotengeneza mistari ya kudhibiti maji kwenye sehemu ya mitiririko na kukata miti.Wakiwa na lengo la kutaka kuongeza uzalishaji,wakulima walitumia mbolea ya kizungu: DAP,MOP na Urea.Kuvuna walikua wakivuna lakini mbolea hiyo ilisababisha ardhi kupoteza rutuba.Katika Kongamano la kimataifa kuhusu mazingira,mataifa yalitoa azimio ya kupunguza utumiaji wa mbolea za kikemikali.Watalamu kwenye maswala la utumiaji mbolea walikuta kwamba mbolea nzuri ni mbolea inayochanganya samadi na madini.Mwaka wa 2019 ndipo inchini Burundi kulianzishwa kiwanda FOMI ambacho kinatengeneza mbolea asilia inayochanganywa na madini.Toka wakati huo hadi leo wakulima ambao walitumia mbolea hiyo walishajionea jinsi ilivyoweza kurudhisha rutuba ardhi zilizokua zimeipoteza.Wakulima wa mikoa ya Butanyerera na Gitega ambao tuliwatembelea walitoa ushuhuda wao kwamba mbolea inasaidia kuongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa.Wanaeleza pia kuwa ardhi inapata virutubisho ambavyo ilikuwa haipati kutokea ile mbolea ya zamani.Mkuu wa idara ya mazingira,kilimo na ufugaji kwenye mkoa wa Gitega anafafanua kwamba aina mbalimbali ya nyasi zilizokuwa zimetoweka zimeweza kujitokeza tena akibaini kwamba hali hiyo ni baada ya kuwa wametumia mbolea ya FOMI.Kwa niaba yake,FOMI ni nzuri kwa sababu ina kinyesi cha ng’ombe ndani yake na ina virutubisho vingi ukilinganisha na ile ya zamani