Kampuni inayotengeneza mbolea asilia ambayo imechanganyika nayakikemikalo  inchini Burundi FOMI liliitikia mualiko lililopewa na wahusika wa utawala wakishilikiana na wahusika wa kilimo,ufugaji na mazingira mkoani Gitega kwenye zoezi la kupanda miti ambayo ni rafiki kwa mashamba Alhamisi tarehe tisa janwari mwaka 2025 ,na shughuli hizo zimefanyika kwenye mulima wa GASIRWA kata ya GWINGIRI tarafani Bugendana  mkoa wa Gitega

Matangazo ya habari
DCIM\101MEDIA\DJI_0872.JPG
DCIM\101MEDIA\DJI_0906.JPG
DCIM\101MEDIA\DJI_0792.JPG
DCIM\101MEDIA\DJI_0919.JPG

Huo mlima unaitwa GASIRWA,sehemu kubwa pake ni wazi,hapajapandwa miti ;ndipo wawakilishi wa Kampuni ya FOMI wakiambatana na Utawala,wahusika wa kilimo ,ufugaji na mazingira nawengineo wengi wakazi wa Gitega wamekutana na raia kwenye zoezi la kupanda mti kwenye mlima huyo wakilenga kutunza mazingira.baada ya shughuli hio,waliokuepo wameshiriki mjadara maana zoezi la namna hiyo ni vyema lifuatwe na ufuatiliaji wa karibu ili miti hiyo iweze kukua vizuri,ichangie kwa kutunza mazingira bila kusahau kuachangia kwa utunzaji ardhi.Kwenye hotuba yake,mkuu wa ofisi inayohusika na mazingira ;kilimo na mifugo Mkoani Gitega Uwikunda Oscar aliishukru Kampuni ya FOMI kwa mchango wake kwenye swala zima la kutunza mazingira ikipititia kwenye mradi wa kuzalisa bustani za miche  na kupanda miti pale ambapo panaonekana kama jangwa

Na Nindemera  Maria,mushauri wa gavana wa mkoa wa GITEGA ambae ana husika na uchumi na utawala, na ambae alikua amemuakilisha mkuu wa mkoa kwenye shughuli la kupanda miti kwenye mlima wa GASIRWA alilishukuru KAMPUNI ya FOMI kwenye shughuli hio ya heshima kando ya kutengeneza mbolea ambao inasaidia uzalishaji kua mkubwa na ardhi kurudisha rutuba yake ,kulinda afya ya watu na viumbe hai.Na kwa maana hiyo anaiomba FOMI kuendelea na shughuli za namna hiyo hata kwenye tarafa zingine mkoani Gitega.

Mkurugenzi wa kilimo kwenye Kampuni FOMI Kanyegeri Cassien alishukuru kwa niaba ya Mukurugenzi mkuu wa FOMI namna FOMI ilivyoalikwa kuja kuungana na wengine kwenye shughuli hiyo na namna Kampuni hiyo inavyoshilikiana vizuri na utawala hata na wahusika wa kilimo,ufugaji na mazingira mkoani Gitega ambaye ndie aliewakilisha ,aliwashukuru wote .Baada ya kuambia kile ambacho FOMI wamesha kitekeleza ili wachangie kwenye mradi wa kutunza mazingira,alitoa wito wake kwa raia wa kuitunza miti hiyo

Raia waliokuepo kwenye zoezi waliishukuru sana Kampuni ya FOMI ilioandaa na kutekeleza zoezi la namna hiyo ambalo litapelekea ardhi yao kuota na kujikinga na mitiririko ya maji .Na waliitikia kuitunza miti hiyo kama walivyoombwa.

Kwenye mradi wa FOMI wa kutunza mazigira ,wawakilishi wa FOMI wakiongozwa na mkurugenzi wa kilimo kwenye KAMPUNI ya FOMI Cassien Kanyegeri zilifika pia ;siku hiyo hiyo mkani Kayanza,tarafani Muhanga sehemu kuna shamba la miti ilipandwa miaka miwili imeisha tayari ;Cassien Kanyegeri ambae anahusika na kilimo kweye FOMI anashukuru kwa hari alioyikuta akichukulia kile ichokiahidi FOMI kwenye swala la kutunza mazingira na akachukulia na fasi hiyo kueleza faida za mradi huyo kwa mtu kwa ujumla

Raia wanashukuru mfano mzuri wa FOMI kwenye swala la kutunza mazingira. Kwa maoni yao,miradi hiyo ni vyema ikasapotiwe ili na semu zingine ziweze kunufaika kama inavyothibitishwa na mwalimu wa kilimo

Kwenye  Zoezi la kutunza mazingira,Kampuni ya FOMI inauzoefu ndio maana imeshapatiwa visibitisho kwamba inaweza na kwamba inafanya vizuri si kwa ngazi ya kitaifa pekee bali na yakimataifa kile kinachoitwa ISO 14001 kama inavyofafanuliwa na MANYANGE Hermenegilde Makamu mukurugenzi mkuu wa FOMI Mutafahamu kuwa kampuni ya FOMI lilikubali kuendelea likiitia wito huo wakuendelea kuunga mkono shughuli hizo za kutunza mazingira,wakiwa na malengo ya kuenda na kaulimbiu ya inchi iliondelea mnamwo mwaka wa 2040  na inchi tajiri mwaka wa 2060