Kiwanda kinachotengeneza mbolea ya asilia ambayo imechanganyika na ya madini FOMI, kwa mda ambao kimemaliza kikitengeneza mbolea yenye ubora wa kipekee, inayowezesha uzalishaji kuwa mkubwa na kurudisha rutuba ya ardhi, kinasaidia pia watafiti wenye lengo la kuendeleza au kuboresha ujuzi wao. Kwa sasa,kiwanda hicho kiko kwenye hatua ya kupokea watafiti wanaotokea inchi zingine. Hiyo ni ishara nzuri inayothibitisha uhusiano mzuri kati ya Burundi na inchi za kigeni.
Pauline WAMBUI MIGAI ni mtafiti kutokea Kenya, ni mwalimu kwenye chuo kikuu cha Masinde Muliro University of science and Technology, alikuja kufanya utafiti hapa kiwandani FOMI, anatueleza kuhusu utafiti alioufanya na kwa nini alifanya utafiti huo.
Pauline : Nilikuja kufanya utafiti kuhusu mbolea mbolea asilia tukitumia takataka, mbolea ambayo inaweza ikusaidia wakulima wadogowadogo.Nilikua hapa FOMI nikiboresha ujuzi kuhusu utengenezwaji wa mbolea asilia na kutafuta kuzijua changamoto wanazokutana nazo katika kutengeneza mbolea hizo.Nilijifunza pia kuhusu ubora wa mbora hio na kuhusu virutubisho tunavyokuta kwenye mbolea hiyo.
Pauline MUIGAI anasema kwamba kilichopelekea akachagua kufanyia utafiti wake katika kiwanda cha FOMI ni kwa sababu kina vifaa vya kisasa na vyenye uwezo mkubwa na watalaamu wzenye uwezo.
Kilichopelekea nikachagua kufanyia utafiti wangu hapa FOMI, FOMI inawataalamu walionisaidia kwenye shughuli zangu za utafiti; ina mabara ya kisasa yenye vifaa tosha ili mtu aweze kuchunguza kama mbolea inavigezo tosha au hafifu kwenye mmea. Vilinisaidia sana.
Mtafiti huu anaeleza pia kile ambacho utafiti alioufanya FOMI unaenda kumsaidia
Kama mtu mwenye mradi wa kuangalia kama ardhi inaweza kurudisha rutuba yake, kujifunza na kuwez akupata maarifa ya kutengeneza mbolea, ninaimani nitaweza kuyatumia kwenye inchi yangu ili takataka hilo tuweze kunufaika nalo kwa kulitengenezea mbolea. Kwa upande mwingine kama mwalimu,nitaweza kufundisha watu namna ya kunufaika kwa kupata mbolea ukitumia takataka ambayo unakuta imezagaa hapa na pale.
Gustave nkurunziza ni mhusika wa kitengo cha kuunda vipyaa kwenye shirika la FOMI na ndie aliesaidia huo mtafiti kwenye utafiti wake, anaeleza kwa kifupi jinsi shirika la FOMI lilivyosaidia mtafiti na ni nini faida kwa FOMI kuwapokea watafiti.
Alikuja kupitia mradi unaotekelezwa kati ya inchi za Burundi, DRC na Kenya amnbao unaungwa mkono na shirika la Bio innovate Afrika kwenye kitengo chake cha kuendeleza utafiti unaofanwa na wanawake kwa hapa kanda ya Afrika mashariki. Ni mradi ambao unalenga kutengeneza mbolea ya aina ya kikaboni, mbolea ya Biofertilizer inayopatikana kwa kutumia wadudu( bacteria) wanaosababisha kuingiliana kati ya mmea na ardhi ambapo wadudu hao wanapatia mmea Nitrojeni na mmea kuoa kaboni kile tunachokiita Isobiamu na hatimae tunachanganya na kivu ya ardhini vijulikanavyo kama mikolysis ili mmea uweze kustahimili vizuri ni kwa maana hiyo alikuja kushilikiana na FOMI kwenye utafiti wake. Utafiti anaoendesha akiungwa mkono na kitengo chetu unaenda sambamba na kile kinachofanyika hapa hapa FOMI kwa kua FOMI inatengeneza mbolea asilia ambayo imechanganywa na ya kimadini ambayoinaitwa ” Organo Mineral” hivyo tunahitaji sana mbolea asilia ikiwa ni ile itokayo kwa mifugo au ile inayotoka kwenye takataka ambayo haina hitirafu; kwa hiyo Biofertilizer ambayo tuko tunajaribu kutengeneza kwa hapa Afrika Mashariki inatengenezwa kwa kuunda vizuri takataka kama alivyoeleza mwenyewe kwa hiyo vinaambatana sana na kitengo ninachokisimamia na kile tunachokifanya FOMI kwa sababu itakuja kusaidia kwa hiyo mbolea asilia ambayo inahitajika sana kwa hapa na kuleta manufaa kwa maana katika shughuli zetu kuna pia kuunda vipya ikiwemwo na hayo mahitaji ya kila siku yanayotuwezesha kutengeneza mbolea ya FOMI, kwa hiyo mchango wake kwa hapa utafiti ni kwamba tutapata kitu kingine ambacho kitaweza kusaidia na chenye ubora
Paulina : Ujumbe kwa viongozi wa FOMI nawashukuru sana kwa kua waliruhusu watu wenye nia ya kujifunza na wale wanaoendesha utafiti kuhusu namna ya kutengeneza mbolea,nawashukuru watu wote waliounga mkono utafiti wangu. Ninawaomba FOMI waendelee kuwapokea na watafiti ambao watakuja nyuma yangu ikiwa niwahapa inchini hata na wale wakutokea mataifa mengine kama walivyonifanyia mimi.
Gustave Nkurunziza anajurisha kuwa kwenye kitengo anachokiongoza utafiti ni jambo endelevu, anaomba huyo mtafiti Paulina MUIGA kutumia vizuri alichojifunza hapa FOMI na kama itampendeza kurudi ili aendelee kuingia ndani zaidi na kuweza kufanikiwa kwenye mradi wake ili na utafiti kwenye FOMI uendelee kupiga hatua kwenda mbele
Ninachoweza kumshahuri na nilishamshahuri tayari ni kuendelae kuwa na bidii kwa kuendelea na shughuli zake kama alivyokuwa akifanya kwa miezi mitatu ambayo tumekaa nae na kuendelea kushilikiana na team ya hapa FOMI na team ambayo wako nayo ili tuendelee kuendeleza tekenolojia hiyo.Nilimshahuri pia kwamba itapendeza tukiweka kwa pamoja tekenolojia walionayo hapa na tekenolojia walionayo Kenya kwa sababu sote tuna nia ya kuendeleza kilimo kwa mkulima wa kanda hii ili apate chakula tosha bila kuchoka. Ushahuri nimempa ni kuweka kwa pamoja tekenolojia tunabahati hicho ni kitu anchokielewa na yeye ili tuendeleze Afrika mashariki na kanda nzima na hilo ni wazo la mashirika yetu ya ITRACOM Fertilizers ya kupanua maeneo ni vyema pia tukapanue na utafiti na tekenolojia tuvichangie sote