Ziara ya wanajeshi wa ECBEM kwenye kiwanda cha FOMI.


Wanajeshi kutoka kwenye kundi la uongozi na uongozi wa ngazi ya juu jeshini wamefanya ziara Juma inne hii 24 June 2025 kwenye kiwanda cha FOMI.

Kwenye neno lake la ukaribisho,makamu Mukurugenzi mkuu wa FOMI aliwafafanulia kwa kifupi Kiwanda cha FOMI na huduma zake na hatimae akawaalika kufuata dokimentari mbili,moja kuhusu ufafanuzi wa ni nini FOMI,malengo ya uundwaji wake mwaka 2019,mbolea zitengenezwazo,uwezo wake wa uzalishaji,utaalamu wanao utumia,upanuaji wake na muelekeo wake wa mbeleni ili waweze kutosha uhitaji kwa hapa Burundi,Afrika na ulimwengu ya mbolea ya kikaboni na kimadini.
Dokimentari inayoonyesha ziara kubwa ambazo viongozi wakubwa wa inchi ikiwa ni wa hapa kwetu Burundi na viongozi wa inchi zingine wameshazifanya kwenye FOMI toka FOMI ianze hadi leo. Ir Manyange Helmenegilde aliwaeleza umuhimu wa mbolea ya kikaboni na ya kimadini ambayo inatengenezwa na FOMI ambayo imevutia ulimwengu ndio maana walipanua kiwanda hata kwa inchi jirani kama Tanzania,kenya,Uganda na kwingineko.Tarehe 28 june 2025 kiwanda ITRACOM fertiliser ambayo ilijengwa Tsnzania itazinduliwa na Muheshiwa Dr Samia Suluhu Hassan akiambata na mwenzake raisi wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania na mwenzake wa Burundi muheshimiwa Meja Jenerali mustafuu,Evariste Ndayishimiye aliendelea akitaja makamu mukurugenzi mukuu bwana Manyange.


Walihitimu ziara yao wakizungukia kiwanda ili washudie namna utengenezwaji wa mbolea unavyofanyika na namna kiwanda cha FOMI kilivyopanuliwa.







