Tutumie vizuri mbolea na chokaa ya kilimo vinavyotengezwa na FOMI,tuongeze uzalishaji,tukichukulia muelekeo wa inchi yenye kasi ya kuendelea munamo mwaka wa 2040 na tajiri mwaka wa 2060


Leo hii tarehe mosi mwaka 2025,ndipo warundi wameungana na inchi zingine kuadimisha siku kuu ya wafanyskazi na kazi.Kwa hapa Burundi,siku kuu imeadimishwa kwa kauli mbiu ifuatayo:”Tuongeze uzalishaji tukizingatia muelekeo wa inchi yenye kasi ya kuendelea munamo mwaka 2040 na inchi tajiri 2060.
Ikichukulia kauli mbiu hiyo ya inchi,kiwanda kinachotengeneza mbolea ya kikaboni ambayo imechanganywa na madini FOMI nacho kimeungana na wengine kuadimisha siku kuu hiyo kwa kauli mbiu ya:” Tutumie vizuri mbolea na chokaa ya kilimo vinavyotengezwa na Fomi FOMI,tuongeze uzalishaji,tukichukulia muelekeo wa inchi yenye kasi ya kuendelea munamo mwaka wa 2040 na tajiri mwaka wa 2060.

Sherehe kwenye ngazi ya inchi zimefanyika mjini Bujumbura kwenye Kiwanja cha michezo Intwari stadium ambapo shere nyingi zimefangika zikianzishwa na gwaride ndefu ya wafanyakazi kwenye segita za kikazi mbalimbali

Wafanyakazi kwenye kampuni ya FOMI ambao wamewakilisha wengine kwenye sherehe hizo walikuwa wakionekana kuwa na furaha inayoonyesha kwamba FOMI imezingatia kutimiza wajibu wake wa kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa kilimo kwa kuwapatia mbolea kabambe ya kuwezesha uzalishaji kuwa mkubwa,kurudisha rutuba ya ardhi na kutunza mazingira ili Burundi iweze kuyafikia malengo yake ikipitia kilimo.

Kwenye hotuba yake ,Raisi wa jamuhuri Mheshimiwa Meja Jenerali Evariste Ndayishimiye alisisitiza kuhusu kuongeza uzalishaji,kuunda utajiri mpya kila siku huku akiwashukuru wafanyakazi wanaotumia mda vizuri.Tukomeshe tabia ya kudharau kazi maana mdharau kazi hufa masikini.Alimaliza hotuba yake akitakia wafanyakazi na watoakazi kila la heri.
Baada ya sherehe,wafanyakazi wa FOMI wameendelea sherehe makao makuu ya FOMI ambayo yako kata ya Maramvya,tarafani Mutimbuzi ambapo wamechangia siku kuu vinywaji na mlo na matawi mengine ya ITRACOM HOLDING navyo ni vifuatavyo ITRACOM ambayo inahusika na Transportation,FOMI ambayo Burundi ambayo inatengeneza mbolea hapa Burundi,ITRACOM Fertilizers ambayo inatengeneza mbolea Tanzania,INKINZO ambayo inahusika na insurance,Benki ya wakulima BCAB,ITRAPACK ambayo inatengeneza mifuko ya kubebelea ambayo ha
yiathiri mazingira na ITRASAGRI amayo inazalisha mbegu bora huku wakifurahi pamoja na muanzirishi wa ITRACOM HOLDING muheshimiwa Ntigacika Adriano.

