Ardhi yetu ilipoteza rutba na ikapelekea uzalishaji kuwa mdogo ukilinganisha na hali ilivyokuwa zamani ambapo tulikuwa tukivuna vizuri bila kutegemea mbolea . Miaka sita imetimia tayari wakulima wa inchini Burundi wakitumia mbolea ya FOMI ambayo imetengenezwa kwa mchanganyiko wa mbolea ya samadi na ya kikemikali. Hiyo mbolea ya FOMI ilishaonyesha kwamba ni bora kwa kuwezesha uzalishaji kuwa mkubwa,ardhi ilioharibika kurudisha rutba na kutunza mazingira na wadudu hai vinavyowezesha ustawi wa mimea.Je nini kinachoifanya mbolea ya FOMI kuwa ya kipekee ? imetengenezwa kwa madini gani na zina umuhimu gani kwa mazao , kwa afya ya watu na ardhi iliyokwishaharibika kwa sababu ya asidi ilioandama ardhi sehemu mbalimbali ?
Kampuni inayotengeneza mbolea asilia ambayo imechanganyika na ya kikemikali FOMI imetimiza miaka 6 ikitengeneza mbolea yenye kutumika kwa mazao mbalimbali. Kuna FOMI IMBURA ambayo inatumika kwa mazao yote, FOMI BAGARA inatumika kwa mazao yenye mizizi na FOMI TOTAHAZA ambayo hutumika kwenye mazao nafaka. FOMI IMBURA na FOMI TOTAHAZA hutumika pia wakati wa kupalilia kulingana na aina ya mazao. Mwalimu wa chuo kikuu na mtafiti kwenye maswala ya kutumia mbolea profesa KABONEKA Salvator anaeleza kwamba namna mbolea ya FOMI imetengenezwa inawezesha ile ardhi iliopoteza rutba yake kupata virutubisho vianavyoyiwezesha ardhi kurudi kwenye hali yake yazamani hivyo mazao nayo yanapata virutubisho vya kuyasaidia kukuwa vizuri na uzalishaji kuwa mkubwa.
• Angalia namna ardhi ilivyo, upande wake wa kikaboni na upande wake wa madini kwa chini Katikati pake ukitaka kuna kitu kinaitwa upeo wa mchanganyiko yenye upeo wa kikaboni wa juu juu na upewo wa madini kwa chini ndio muonekano wa ardhi. Kwa hiyo ili turudishe ardhi kama ilivyokuwa mwanzo kabla ya mwanadamu kutumia virutubisho vyake na kuyicha masikini lazima turudishe virutubisho vilipelekwa kungine hicho ndicho tunakiita kanuni ya kurudisha na nikitu ambacho hakifanyiki. Hilo ni le kwanza.2. tupaswa kurudisha,kuunda,kuzaa upya upewo wa kikaboni tufanye kama Mungu alivyofanya na tunafanya je? Tunaleta vitu vya kikaboni,Samadi, unaleta vitu vya madini unaviweka kwa Pamoja, ukiwa umeviweka kwa Pamoja unapata mbolea inaitwa ya kikaboni na ya kimadini kwa maana ya FOMI.
Sayansi inatwambia ili mmea aweze kuzaa matunda Pamoja na kaboni ambayo inapatikana katika dioksidi ya kaboni na haidrojeni na oksijeni ambavyo vinapatikana kwenye maji, mmea lazima upate virutubisho kutoka ilimenti 13. Kuna kanuni,hiyo . lakini ni vitu kumi na tatu. Leo, virutubisho vitatu DAP inaleta mbili ambavyo hujazwa na Nitrojeni kutoka kwa Urea kwenye orodha ya virutubisho ambavyo mmea unahitaji. Ni mbali…bado ni mbali. Mbali na athari ambazo sio nzurizinazosababishwa na mbolea ardhini na uhai wa ardhi.
Hatua: virutubisho viwili vya nyongeza vinavyoletwa na FOMI: Kalisiyamu na maginesiamu. Kulingana na changamoto ya aside ambayo inaondoa uwepo wa virutubisho kwenye ardhi.Toka tatu nenda tano. Kwa mshangao nimeambiwa kwamba tukichukulia majibu ya uchambuzi uliofanyika kwenye mabara Urayani hususani Ubeligiji Kwamba mbolea ya FOMI inavirutiubisho vingine vinavyoitwa vipengee vidogo ambavyo vina kazi nyeti ya kuwezesha ukuaji wa mmea.
Ni nini tunakikuta katika mbolea ya FOMI? Kuna molybdenum. Nikifafanua kidogo molybdenum inawezesha uwepo wa nitrojeni kwenye kunde,soya,maharage vyote hivyo.Kwa hivyo molybidenum kiberiti,shaba,zinki nikifafanua kidogo Zinc na shaba ndivyo virutubisho haba sana kwa kipi cha hapa karibu hapa Burundi.
Kwa maana nyingine virutubisho vitatu kwa jana, vitanu kwa leo na endapo uchambuzi ukidhihirika vitanu Kwenda tisa ndani ya mbolea ya FOMI nakwambia ni hatua kubwa ambayo ni ya kufuata na kuunga mkono na muelekeo ukiwa ni kuwa na kumi na tatu ni procesi kwa mfano tukichukulia kesi ya FOMI, FOMI hayileti Nitrojeni,fosforasi na potasiamu.Kwanini tuyichukulie na tuyilinganishe na DAP,Urea na KCL ambazo zinareta virutubisho viwili au kimoja.
FOMI inaleta Kalisiamu, maginesiamu kwanini tusithamini virutubisho hivyo? Kuwa na virutubisho mbalimbali kwenye mbolea ndio malengo kwasababu tunajuwa idadi ya virutubisho ambavyo mmea unahitaji. Kirutubisho kimoja hakitoshi, virutubisho viwili havitoshi,virutubisho vitatu havitoshi hakika havitotosha kama virutubisho vitanu ambavyo tunakuta vimo katika utengenezwaji wa FOMI.
Tutakuwa tumetibu ardhi yetu pale ambapo tutakuwa tumeyirudisha kwa hali yake ya zamani kwa kuyipatia mbolea ya samadi ambayo imechanganyika na ya kikemikali FOMI. Mbolea ya FOMI sasa ndivyo ilivyotengenezwa na ndicho kinachopelekea mbolea hiyo kuwa ya kipekee ukiyilinganisha na ile ya iliotumikishwa toka zamani ya kikemikali. Mbolea ya FOMI kwa sababu ya samadi walioyiweka na virutubisho huongezeka.
• Kiukweli DAP na Urea hazikupashwa kuwekwa kwenye ardhi bila kuziambatanisha na chokaa ya kilimo,kalisiamu na maginesiamu ili kupunguza aside inayoendana na mbolea hizo ili tusiweke ubaya juu ya ubaya kwa kuleta aside kutoka kwa mbolea kwa aside tunayokuta kwa udongo. Nawambia Kalisiamu na maginesiumu ndio jibu kuziweka Pamoja ndicho FOMI inachokifanya. Hizo microorganism ambazo hatuzitambuwi na hatuzioni ni kaboni. Kaboni inapatikana kwenye vitu vya kikaboni.
Kwa hiyo unapoweka mbolea ya kimadini pekee Nitrojeni ,fosforasi na potasiamu mwaka baada ya mwingine mmea unahitaji kaboni na hauupatii kaboni kwenye mbolea hiyo,na mwili unahitaji kaboni unawutafuta kwenye vitu vyenye kaboni. Inakula….inakula kitu cha kikaboni.
• Pamoja na mchango wakimadini,inakula mpaka kumaliza kaboni na kaboni munayoifahamu hicho ndicho muzunguuko wa maji,muzunguuko wa hewa hicho ndicho tunakiita uwezo inamaana hizo microorganism zinakula kwa kiasi kikubwa madini ambayo mumeyaleta kwa kuweka mbolea ya kimadini, imekula na kumaliza kaboni ya ardhi na munapoteza vielelezo kama vya muonekano,kikemikali,biologia muna ardhi iliojifunga,ngumu na huyo ndio ukweli. Ambatanisheni mbolea hizo na vitu vya kikaboni kwasababu ambazo nimetoka kuzitaja na nikiwakumbusha pia kwamba ardhi ni kitu : kaboni na madini.tujuwe asili ya ardhi tafadhali.
Kwa sasa kwa Burundi, ardhi imefulika kwa kiasi cha kuhitaji kupewa virutubisho munapo weka mbolea ya kikaboni mpaka pale ambapo mutarudisha ardhi kwa asili yake una manage ardhi weka mbolea ya kikaboni, hilo linatosha.
Mbolea hiyo ambayo watu wanafurahiya kwa sababu yaubora wake ili iweze kupatikana utafiti ulifanyika. Watalaamu wa FOMI wakishilikiana na watalaam kwenye tasisi ya sayansi ya kilimo hapa Burundi ISABU na chuo kikuu cha Burundi waliithinisha chumvichumvi tunazozikuta kwenye mbolea ya FOMI na ndivyo munavyoona kwenye mifuko ya IMBURA, TOTAHAZA au BAGARA.
• Nilitaka niwambie kwamba tunafanya utafiti wa kilimo tukishilikiana na tasisi ya ISABU ,vyuo tofauti kama Chuo kikuu cha Burundi na vyuo vingine vya kibinafsi vinavyopatikana kwa hapa Burundi na inchi za kigeni. Mbolea ya FOMI ina chumvichumvi nyingi tuchukuwe kama Nitrojeni,Fosiforasi na potasiamu kando ya hivyo kuna chumvichuvi za ngazi ya pili kalisiamu,magineziamu na kiberiti.
Virutubisho vingine vinavyofahamika kwa majina ya Oligo elements ni vine kuna zinki,boroni,shaba na molybdenum. Kwasababu tunatumia Samadi kama malighafi tuligunduwa kwamba na Samadi yenyewe ina Oligo element ni kwasababu hiyo tulitaka kujuwa kiasi cha oligo element kwenye mbolea yetu .
Tulituma samples kwenye mabara maarufu inje kama ubeligiji na majibu yalikuja yakionyesha kuwa mbolea yetu ina aina hiyo ya virutubisho vinavyoitwa oligo element. Ni kwa sababu hiyo tuliwaza kuchunguza uwingi wa oligo element kwa mbolea yetu.
Sample ya mbolea ya FOMI iliopelekwa mabara ilionyesha kiasi cha virutubisho vinavyofahamika kwa majina ya origo element ambavyo vimo dani ya FOMI toka mwaka wa 2019. Kitu cha kuzingatia na cha kujivuniya ni kwamba mbolea hiyo inatengenezwa na warundi wenyewe.Muanzilishi wa FOMI alionyesha kuwa alielewa mapema mpango wa inchi wa kuendeleza kilimo.
• Bwana NTIGACIKA Adrien aliyeelewa mapema kwamba kwenye segita ya kilimo kitu cha kwanza kinachohohitajika ni mbolea kwa sababu kulima bila kuweka mbolea ni kupoteza muda.Majuzi kati nilikuwa nimeenda kutembelea kiwanda chake ili nione utaalamu wanaoutumia tukakuta vifaa ni vya kutosha,mashini kubwa kubwa ambazo alieleza kuwa zimenunuliwa inje maana kwa hapa Burundi hazipo.
Alitueleza kwamba wakati wa manunuzi kila kifaa kilikuwa kinajitegemea kwamba watalaamu warundi ndio waliviambatanisha.Nahisi kuwa watu tulioongozana nao mulishudia kuna mashini zingine zinafanya hiki,zingine zinatwanga kile ilikuwa ni mazingira ya kufurahia.
Munaona kwamba jitihada kama ile ni ya kuungwa mkono. Tungepata wawekezaji wabunifu wengine inchi yetu inaweza kuendelea kwa haraka
Raisi wa inchi anafahamisha kama huyo alieanzisha FOMI ni wakuungwa mkono na serikali kwa sababu wanachangia kwa maendeleo ya inchi.
• Kwa siku zilizopita,walikuwa wakilima mazao ya kila aina bila kuweka mbolea.Kilawalipokuwa na uhitaji wa mbolea walikuwa wakitumia mbolea ya Samadi na wakati huo majani yalikuwepo kwa wingi.
Tunafurahiya mchango wa warundi kwa segita ya kilimo mpaka wanajitengenezea mbolea ya mchanganyiko wa Samadi na ya kikemikali ili kupunguza aside ambao inayiathiri ardhi yetu,inayowezesha uzalishaji kuwa mkubwa,afya ya watu kuwa nzuri,kuheshimu mazingira na wakulima wanapata mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu na wafugaji wamepata soko ya Samadi ya mifugo yao.
Wakulima waliotumikisha mbolea hiyo wanashukuru wakisema kuwa mavuno yaliongezeka na kuwa ardhi ilirudisha rutba yake pale ambapo walishaitumia mbolea hiyo. Wahusika wa kilimo kwenye mikoa mbalimbali wanashukuru ubora wa mbolea ya FOMI
• Kampuni ya FOMI inamchango mkubwa katika ku supply mbolea. Tunajivunia uzalishaji tulionao leo na tunapongeza sana wale wote waliowezesha ufanisi huu ikiwemwo na Kampuni ya FOMI iliotoa mbolea kwa wakati ili kilimo kiende vizuri.
• 2 .Kwa sababu ya ardhi kwisha haribika,kuna aina ya nyansi zenye kuonyesha kwamba ardhi ina rutba zilikuwa zimetoweka kwa mfano Icanda ni nyasi ambayo huota kwenye sehemu yenye rutba hiyo inamanisha kuwa mbole ya FOMI baada yakutumikishwa nyasi zenye kuonyesha kurudi kwa rutba huota,ni mfano kama nyasi ya urutezateza ambayo hayiwezi kuota kwenye ardhi iliochoka.kielelezo kingine cha ardhi iliorudisha rutba yake ni rangi ya udongo ambayo inageuka kuwa nyeusi n ani kwasababu ya mbolea ya FOMI inayowezesha ustawi wa mimea.
• mbolea hizo zimeundwa na vipengele viwili : sehemu ya Samadi na majanimajani na sehemu ya madini. Huo mchanganyiko ndiyo unaifanya mbolea ya FOMI kuwa nzuri na kuzalisha kwa ukubwa na uhitaji wa mbolea unakuwa siku hadi nyingine na hilo linadhihirisha wakulima kufurahiya FOMI
• Umuhimu wa kutumia mbolea ya FOMI haswa utumiaji wa chokaa ya kilimo,mambo alibadilika kwasababu hapa kulikuwepo nyasi ziitwazo ishinge na hizi huota kwenye ardhi iliyoharibika,hizo nyasi kwa shamba hili hazipo tena zimebadilishana na nyasi kama Icanda,Ikurasuka,imibebe hiyo inamaanisha aside ilitoweka
• Mchango wa mbolea ya FOMI unaonekana kwa uzalishaji wa kilim oni ukweli kwamba mukulima asipoweka mbolea mazao hayatokuwa mazuri.Inafikia wakati zao la muhindi inafikia kipindio cha mavuno bila hata kuwa na urefu wa mita moja. Kinyume chake unapotumia mbolea haswa FOMI imbura ambayo inasaidia mumea kukuwa na afya unapoheshimu kiasi stahiki kama inavyoelekezwa na watalaamu wa kilimo lazima mavuno yawe mazuri.
• Pamoja na mbolea ya FOMI unaona kuwa ardhi inatoka kuwa nyekundu Kwenda kuwa nyeusi. Tunapolinganisha mashamba hayo mawili ya majaribio,tunaona kwamba mavuno yatakuwa tofauti tutavuna zaidi pale ambapo tuliweka mbolea ya FOMI kuliko pale ambapo tuliweka mbolea ya zamani
• Mbolea ya FOMI hayiharibu ardhi ndio maana tunayisifu sana.Tuliweka mbolea ya zamani sambamba na mbolea ya FOMI kwa sababu tulikuwa tunalenga kuonye utofauti uliopo mbeleni hatutotumia mbolea ya zamani tena kwa sababu tulishajionea uzuri wa mbolea ya FOMI. Angalia muhindi huu ulivyo, ni mzuri mno.
• Hakika,tumefurahi, hizi mbolea ni zamuhimu, itakuwa ni shida kubwa ya uzalishaji tusipopata mbolea hii, Tunaponhgeza kampuni ya FOMI kwa kuwa walifanya kila liwezekanalo ili wakapate namna ya kuongeza uzalishaji na ni kweri tulipiga hatua mwaka huu tulizalisha kuliko mwaka jana.
• Mbolea ya FOMI ni za muhimu sana,tunaona kwamba utumiapo mbolea ya FOMI ardhi inakuwa nyepesi ya kumimina maji na kuweza kusalimika kipindi cha uhaba wa mvua.Unaweza ukawa na mashamba mawili kwa sehemu mmja ambayo hayiwezi kuvumilia sawa wakati wa ukame ni kwa sababu shamba lenye mbolea ya FOMI linastahimili kiasi kwamba utafikiri wanalimwagilia. Mbolea ya FOMI ni muhimu sana.
• Hapa tuliweka DAP,KCL na Urea mbolea za zamani ardhi imeharibika,ardhi ya upande mwingine imejirudiria.
Tujifunze kujivunia tulichonacho.Hata hivyo warundi wengi walishajionea kwamba mbolea ya FOMI ni muhimu kwa kuwezesha uzalishaji kuwa mkubwa. Na wageni walisha vitiwa na mbolea hiyo na wakaomba kampuni ya namna hiyo kuwepo makwawo. Ebu tukimbilie ya kwetu, tukimbilie mbolea yetu ya FOMI. Mungu awabariki