Muwekezaji Adrien Ntigacika alipokelewa na Mheshimiwa Doctor Samia Suluhu Hassan Rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania.



Huyu alieanzisha kiwanda kinachotengeneza mbolea ya kikaboni na Madini FOMI inchini Burundi mwaka 2019 na hatimae akapanua mradi kwa kuanzisha kiwanda kama hicho nchi jirani ya Tanzania,alipokelewa na muheshimiwa rais samia Suluhu Hassan tarehe 28 May 2025. Walizungumza kuhusu miradi ambayo iko inatekelezwa na Fomi inchini tanzania na nini cha kufanya ili kuongeza uwingi wa mbolea inayotengenezwa Tanzania. Adrien Ntigacika mkuu wa ITRACOM Holding alikua ameongozana na mukurugenzi kwenye Itracom Fertilizers Ltd,bwana NDUWIMANA Nazaire. Miradi inayotekelezwa na Adrien Ntigacika inachangia kwa kudumisha uhusiano na kuendeleza uchumi kati ya Burundi na Tanzania.

Kwenye miradi yake yakuendelea kupanua uwekezaji wake kupitia kuanzisha viwanda kwenye inchi zingine,Adrien Ntigacika alimutuma musaidizi wake bwana NIYOYANKUNZE Méthoucellah inchini Ghana. Kwenye ziara hiyo ya kikazi, inchi ya Ghana ilikubali kutoa kiwanja ambapo kutajengwa kiwanda cha FOMI. Itafahamishwa kuwa bwana Méthoucellah, alionana na naibu waziri wa kilimo inchini Ghana. Hapo, pamoja na inchi zingine wako wanakimbilia mbole ya FOMI kwa sababu inapelekea uzalishaji wa kilimo kuwa mkubwa, kurudisha rutuba ya ardhi kama ilivyokwisha shuhudiwa kwa hapa Burundi,Tanzania na kwingineko.